Featured Posts

May 14, 2016

YNA WA THE PROMISE AJIKITA KUMCHA MUNGU NA KULEA FAMILIA YAKE, AWEKA PEMBENI UIGIZAJI.

Mwigizaji nyota wa Ufilipino ambaye ameokoka, Kristine Hermosa almaarufu kama YNA katika tamthilia ya The Promise, ameamua kujikita zaidi na familia yake baada ya kutangaza anatarajia kupata mtoto wa tatu katika ndoa yake na mwigizaji mwenzake Oyo Boy Sotto.


Mwigizaji huyo aliamua kutangaza ujauzito wake mpya hivi karibuni, wakati ambao mashabiki wake walitegemea kumuona akirudi tena kwenye uigizaji baada ya mtoto wake wa pili aitwaye Kaleb Sotto kuanza kutembea. 
Aidha mashabiki hao walikuwa na imani ya kumuona mwanadada huyo amabye yeye na mumewe ni wafuasi wazuri wa wokovu, baada ya mpenzi wake wa zamani ambaye kwasasa ni mume wa mtu Jericho Rosales almaarufu kama Angelo kuwa tayari kuigiza tena na Kristine na kwamba wanatarajia jambo hilo kutokea karibuni.


Hata hivyo msimamo wa binti huyo kuweka familia yake mbele dhidi ya fani yake umepokelewa na kupongezwa na wengi licha ya kuumia kumkosa kwenye uigizaji, wakidai kwamba ni msichana wa kuigwa nchini humo kutokana na tabia nzuri aliyonayo, na kuachana na umaarufu na kuweka mbele familia yake. 
Kristine na mumewe Oyo wamejaaliwa watoto wawili mpaka sasa kwenye ndoa yao pamoja na mtoto mwingine wa kiume waliyemchukua kutoka kituo cha watoto yatima ili kumlea, na kufanya kuwa na idadi ya watoto watatu mpaka sasa huku mtoto mwingine yupo mbioni.

Source: GospelKitaa

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.