Featured Posts

June 23, 2016

ANGEL BENARD AFANYA COLLABO NA MWIMBAJI MKALI WA KENYA.

Mrembo na mwimbaji wa nyimbo za injili hapa nchini,  Mwanadada Angel benard anaetamba na wimbo wake mpya "Salama", ambao kiukweli umegusa maisha ya watu wengi ndani na nje ya nchi. 

Jana kuna baadhi ya picha zilisambaa katika mitandao ya kijamii na kuacha maswali mengi katika vichwa vya mashabiki na wapenzi wa nyimbo za injili. 
Baada picha izo za Angel Benard akiwa na Mercy Masika "Mkenya,  Pia mshindi wa tuzo za Groove katika vipengele vitatu tofauti" katika studio za Still Alive nchini Kenya, Angel Benard amekiri na kusema kwamba wamerecord wimbo pamoja na mshindi huyu wa tuzo za Groove.
"My sister and friend in Christ  Jesus. @mercymasikamuguro. Leo katika studio za Still Alive in Nairobi mara tu baada ya kumaliza kurekodi wimbo pamoja. Umekuwa wakati wa baraka sana." Alisema Angel Benard Kupitia Fan page yake ya facebook.
By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.