June 1, 2016

Historia fupi ya maisha ya Goodluck Gozbert.

Goodluck Gozbert amezaliwa tarehe 12/04/1990 katika hospitali ya Bugando huko Mwanza akiwa mtoto pekee wa kiume wa Marehemu Gozbert Rweyemamu na mama yake Janeth Gozbert.

Goodluck alilelewa na mama yake tu kwani baba yake alikufa akiwa na umri wa mwaka mmoja.

Goodluck alianza shughuli za uimbaji mwaka 2005 akiwa na Tumaini Choir (K.K.K.T-Imani) mwanza, na kuanza kuimba pekee yake mwaka 2008Alitoa album yake ya kwanza Agosti 19 mwaka 2008,  aliyoifanya chini ya Ujumbe records.

Mwaka 2012 alirekodi album yake ya pili aliyoipa jina la “Nimeuona” moja ya nyimbo zilizomtambulisha vyema. Ukiachana na kuimba Goodluck Gozbert ana uwezo wa kupiga vyombo mbalimbali vya muziki kama kinanda, guitar, drums na tarumbeta.

Isikupite hii: Historia fupi ya maisha ya Jennifer Mgendi.

Pia Goodluck ni mtayarishaji wa muziki (Producer), mwandishi wa nyimbo, script, mwongozaji wa filamu na muigizaji. Kwa sasa Goodluck anatamba na album yake mpya ya Ipo Siku ambayo aliizindua kwenye tamasha la Pasaka la mwaka huu huko kanda ya ziwa.

Goodluck ni moja kati ya wasanii wachache wa kiume wa nyimbo za injili ambao wamewahi kushinda tuzo za kimataifa ambapo alichukua tuzo ya mwimbaji bora wa kiume na wimbo bora wa mwaka kwa upande wa Tanzania akiwapiku waimbaji kama Boniphace Mwaitege, Enock Jonas, Christopher Mwahangila na wengineo.

Goodluck pia anasifika kwa kuandika nyimbo kadhaa zinazotamba kwenye bongo fleva akiwaandikia wasanii kama Baraka da Prince na Mo Music