June 2, 2016

Christina Shusho ashinda tuzo (kenya) kama msanii bora wa Afrika Mashariki.

Mwimbaji wa injili  nchini Tanzania Christina Shusho ameibuka kidedea kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za groove za huko nchini Kenya kwenye kipengele cha msanii bora wa Afrika Mashariki na kati kwa mwaka 2016.

Shusho amepata tuzo hiyo baada ya kuwashinda kura wapinzani wake kutoka Uganda na Burundi pamoja na John Lisu ambaye pia alikuwa anaiwakilisha Tanzania.
Kilele cha tuzo hizo zimefanyika leo (Jana) mchana huko nchini Kenya. Sio mara ya kwanza kwa Shusho kupokea tuzo za groove na tuzo zingine za kimataifa na inaaminika ndiye mwimbaji wa nyimbo za injili aliyeipeperusha bendera ya Tanzania kwenye tuzo nyingi za kimataifa.