June 7, 2016

Israel wametengeneza kamera ya kugundua magaidi.

Israel wamegundua aina mpya ya kifaa chenye uwezo wa kumtambua magaidi, kwa kuwaangalia tu uso. 

Kampuni hio ya "Faception" iliyopo nchini Israel inasema technolojia hii ina uwezo wa ku-scan uso wa mtu mara moja na moja kwa moja itaeleza wasifu wake wote.
Mintpressnews.com wameripoti hivi "Kwamba technolojia hii itawezesha makampuni ya usalama kwa kuchunguza na kuwajua magaidi na wahalifu kabla ya kupata nafasi ya kufanya madhara, na kampuni hii tayari imesha-saini mkataba na Idara ya Usalama, kwa mujibu wa Washington Post."
The Mirror wameripoti kwamba technolojia hii ilipata ufanisi wa kutambua magaidi 9 kati ya 11 ambao walihusika katika mauaji ya Paris.
"Tunawaelewa binadamu zaidi ya uelewa wa mtu mmoja mmoja, Utu wetu unatambulika kwa DNA zetu na mtazamo katika uso" alisema mtendaji mkuu a kampuni hio ya Faception Mh. Shai Gilboa.