Featured Posts

June 22, 2016

HUU NDIO MSIMAMO MPYA WA SERIKALI KUHUSU MISAMAHA YA KODI KWA TAASISI ZA KIDINI.

Serikali imelegeza msimamo wake kuhusu kuondoa misamaha ya kodi kwenye Taasisi za dini badala yake itaongeza udhibiti ili kuzuia mianya ya matumizi mabaya ya misamaha hiyo.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ametoa ufafanuzi huo mjini Dodoma wakati akiongea na vyombo vya habari ili kutoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizotolewa na wabunge wakati wa kujadili bajeti Kuu ya Serikali iliyopitishwa Juzi na Bunge.

Amesema kuwa uamuzi huo wa serikali umefuatia maombi na mapendekezo mbalimbali ya wadau yaliyoitaka serikali iendelee kutoa misamaha ya kodi kwa Taasisi hizo kutokana na umuhimu wake wa kuisaidia jamii kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na taasisi hizo.
"Kwa kutambua mchango mkubwa wa taasisi mbalimbali za kidini katika utoaji wa huduma za elimu, afya, maji; nimeamua kufuta utaratibu nilioutangaza katika hotuba ya bajeti, badala yake serikali itaimarisha zaidi udhibiti wa misamaha hiyo"Alisema Dkt. Mpango
By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa!
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.