June 10, 2016

Historia fupi ya maisha ya marehemu Askofu Moses Kulola.

Moses Kulola, alizaliwa mwezi Juni 1928, katika familia ya watoto kumi, na watano. Alisajiliwa katika shule  ya kwanza mwaka 1939 iitwayo Ligsha Sukuma shule ya misheni baada ya Ligsha, alijiunga na taasisi ya usanifu mwaka 1949

Alibatizwa mwaka 1950 katika Kanisa la AIC Makongoro.

Alimwoa Elizabeth na walizaa watoto 10 ambapo saba bado hai. alianza kazi za kimisionari mwaka 1950 japokuwa aliitwa mwaka 1949 mara tu baada ya kubatizwa. 

Mwaka 1959 alianza kufanya kazi serikalini, wakati huo huo akihubiri Injili katika miji na vijiji. Utumishi wake mkubwa kwa nchi ulifika mwisho mwaka 1962, ambapo aliamua kujitolea moja kwa moja nguvu zake zote, mwili na nafsi. Mwaka 1964 alijiunga na chuo cha kiteolojia na 1966 alitunukiwa stashahada.

Hakuacha elimu pale tu, aliendelea na masomo mbalimbali ambapo alitunukiwa vyeti mbalimbali katika mataifa mbalimbali.

Alihudumu kikazi kwa miaka miwili kama Mchungaji kabla ya kuwa mpentekoste mnamo 1961-1962, alifanya kazi katika kanisa la TAG 1966 mpaka 1991 ambapo aliamua kuanzishaa makanisa Evangelistic Assemblies God (EAGT), ambapo yalifanikiwa kukua kwa kasi kubwa katika nchi za Tanzania, Zambia , Malawi na kwa ujumla kuna makanisa yapatayo 4000 katika nchi mbalimbali yakiwemo makubwa na madogo.

Askofu Moses Kulola alikuwa ndiye kiongozi mkuu wa hayo makanisa elfu nne, huku Askofu Msaidizi wake alikuwa ni Mwaisabila.

Mchakato wa kuongoza makanisa elfu nne si rahisi na kwamba kumefanyika mgawanyiko wa majimbo yasiyopungua 34 ya kazi na kanda tano kwa ajili ya kurahisisha kazi na kila kanda na jimbo lina mwangalizi wake. 

Kwa mujibu wa kitabu cha historia yake Askofu Kulola amezunguka Tanzania nzima tena wakati mwingine kwa kutembea kwa miguu na kwenye mazingira magumu sana kiasi kwamba ni wito mkuu wa MUNGU mkuu alionao Askofu Kulola na kwa miaka zaidi ya 60 amekuwa akihubiri neno la MUNGU.

Maisha yake yote Mungu amekuwa akimtumia katika ishara na miujiza na sisi sote ni maishaidi.

Source: Maisha Ya Ushindi blog.