June 29, 2016

PADRI APIGA MARUFUKU MAHARUSI KUPAKA SHEDO.

Gazeti la Mtanzania limeripoti kuwa waumini wanawake wanaokwenda kufunga ndoa katika kanisa Katoliki Parokia ya Hananasif Kinondoni, jijini Dar es salaam wamepigwa marufuku kupaka rangi ya mdomo “lipstick”  wakati wa ibada ya misa takatifu ya ndoa.

Gazeti hilo limeongeza kuwa uamuzi huo ulitangazwa juzi jioni na  Paroko wa Parokia ya Hananasif Kinondoni jijini Dar es salaam Padri Gasper Mtengeti, wakati wa ibada ya misa ya kumwombea marehemu Rose Michael iliyofanyika kanisani hapo.

Aidha gazeti hilo limeongeza kuwa kutokana na hali hiyo Padri Mtengeti aliwataka wanawake waache kupaka rangi wakati wa misa takatifu ambapo alitoa sababu tatu zinazotokana na Liturijia ya Ekaristi Takatifu (utaratibuwa uendeshaji wa ibada) chini ya kanisa Katoliki.

Padri Mtengeti alieleza sababu hizo kuwakataza maharusi wa kike kujipaka rangi ya mdomo kuwa rangi hiyo inayopakwa huwa inasalia katika chombo kinachobeba divai ambayo kiimani kwa dhehebu hilo ni damu ya yesu kristu.

Sababu nyingine iliyoelezwa kupitia gazeti hilo ni pamoja na kuwa rangi ya mdomo huwa inachanganyika na damu ya Yesu wakati wanapokunywa kitendo ambacho si chema mbele za Mungu, sababu nyingine ni kuwa rangi hizo hubaki kwenye kitambaa cheupe kinachotumika kufuta kikombe cha hostia baada ya kuguswa na midomo.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.