• Isikupite Hii

  June 23, 2016

  Lowasa aeleza kilicho mleta Tb Joshua kipindi cha uchaguzi.

  Aliyekuwa mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa amesema hakuridhika na matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25, na kwa kulijua hilo, ‘watawala’ walimleta rafiki yake kutoka Nigeria, TB Joshua ili amshawishi akubali matokeo. 

  Lowassa alisema baada ya TB Joshua, muhubiri na kiongozi wa Synagogie Church of All Nations, kukaa naye pamoja na viongozi wengine wa Chadema na kumueleza jinsi ‘walivyoporwa’ ushindi, kiongozi huyo wa kidini alichukia na kusitisha azma yake ya kuhudhuria sherehe za kumuapisha Rais John Magufuli. 

  Soma: Alichokiandika Tb Joshua Kuhusu Mh Rais Magufuli.

  TB Joshua aliwasili nchini Novemba 3, siku mbili kabla ya kuapishwa kwa Magufuli, na alienda Ikulu na baadaye nyumbani kwa Lowassa ambaye alitumia muda mwingi wa ziara yake pamoja naye. 
  "Walimuita rafiki yangu TB Joshua, wakaenda wakampokea. Alipokelewa na Rais Magufuli, akapelekwa Ikulu akazungumza na Kikwete, Baadaye akawaambia wamlete kwangu. Kweli akaja nyumbani kwangu, tukazungumza naye. Sitaki kusema mengi sana niliyomwambia, lakini moja, nilimwambia ukikubali yale matokeo ndugu yangu, heshima yako itashuka hapa nchini na duniani kwa ujumla,” alisema Lowassa.
  Lowassa alisema hayo jana alipokuwa akizungumza katika mahafali ya Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Wafuasi wa Chadema (Chaso) katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. 

  Alisema ni kutokana na msimamo na mazungumzo waliyofanya na TB Joshua ndio yaliyosababisha kiongozi huyo wa kidini maarufu barani Afrika kutohudhuria sherehe hizo za kuapishwa zilizofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

  By Chief Hope 

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
  Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.