• Isikupite Hii

  June 10, 2016

  ASKOFU GWAJIMA AMEANZA RASMI MIKUTANO YA INJILI

  ASKOFU GWAJIMA AMEANZA RASMI MIKUTANO YA INJILI

  Askofu Josephat Gwajima wa huduma ya Ufufuo na uzima hivi karibuni anatarajia kuanza mikutano yake ya Injili jijini Dar es salaam,Gwajima ambaye kwa sasa ameanza amchakato wa ujenzi wa kanisa lake anatarajia kuzindulia mikutano yake ya jijini Da es salaam eneo la Mbagala ulio pembezoni mwa jiji la Dar es salaam.


  Akitoa taarifa kwa jamii juu ya mikutano hiyo Gwajima ametanabaisha kuwa mwaka huu baada ya ukimya wa muda mrefu sasa anarudi tena.

  Hapo awali mikutano hii ya Askofu Gwajima anayeaminika kuwa na waumini wengi kwenye kila Ibada zake ilikuwa ikikutanisha maelfu ya watu.Hapa nchini kwa siku za usoni mikutano ya Injili  ya nje kwa ujumla  imekuwa ikifanyika kwa nadra ukilinganisha na namna ilivyokuwa ikifanyika kwenye miaka ya 90, na hata iliyofanyika kipindi cha hivi karibuni imeshuhudiwa ikiwa na mwamko mdogo wa watu unless makanisa ya mahali pamoja yaamue kushirikiana na kufanya mkutano mmoja wa Injili.


  Tunaamini huu ni mwanzo mpya wa kurudisha zile zama za miaka ya 90.

  By Richard Edward

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
  Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.