June 2, 2016

Sirmbezi - sishangai Christina Shusho kumfunika John Lissu kwenye Groove Awards.

Ikiwa yamepita masaa kadhaa baada ya mwanamuziki wa injili nchini Tanzania Christina Shusho kunyakua tuzo za groove katika kipengele msanii bora wa Afrika Mashariki na Kati kwa mwaka 2016, rapa wa Injili Tanzania SirMbezi amesema alitegemea ushindi huo.

SirMbezi ameongeza kuwa hashangazwi na Shusho kuwafunika wapinzani wake hasa mshriki mwenzake tokea Tanzania John Lissu ambaye walikuwa katika kipengele kimoja na wengine tokea Uganda na Burundi.
SirMbezi
"Ni kitu ambacho kiko wazi kuwa Shusho ana base kubwa sana sio Tanzania tu bali hata Kenya ambapo Tuzo hizo zimefanyika, lakini pia aina ya muziki  anaofanya ni common sana watu wanauelewa zaidi ukilinganisha na muziki ambao John Lissu anafanya" SirMbezi aliiambia Timheaven.com 
Download Wimbo: Maisha Ya Wokovu - Sirmbezi Ft Chiefhope.

Licha ya hayo SirMbezi ambaye sasa anatamba na wimbo wake wa Maisha ya Wokovu amemshauri Shusho kutanua mipaka zaidi kwani kuna uwezekano wa kufanya vizuri  kimataifa zaidi ya hapo alipo.