Featured Posts

June 4, 2016

MUASISI WA KITUO CHA TV 'TBN' AFARIKI DUNIA.

Mrs Jan Crouch maarufu kwa jina la Momma Jan mmoja wa waanzilishi wa kituo maarufu cha Television cha Trinity Broadcasting Network (TBN) amefariki jana (juzi, jumanne) nchini Marekani.

Taarifa zilizotolewa na mwanaye, jumanne wiki hii zinasema kifo cha Mooma Jan kimetokana na Stroke na hivyo ataungana na Mumewe Mr Jan Crouch aliyetangulia mbele za haki mwaka jana 2015.

Mrs Jan Crouch amefariki akiwa na umri wa miaka 78, kwa Kipindi kirefu Momma jan amekuwa kipenzi cha wengi na hii ni kwa misingi yake ya ualimu wa Neno la Mungu.

Kwa sasa inaaminika kwamba TBN ndio kituo Bora cha Television duniani na kimefikia nchi nyingi zaidi duniani kote. Momma Jan na Mumewe kwa pamoja walianzisha TBN mnamo Mwaka 1973 toka miaka hiyo mpaka leo TV hiyo imepitia hatua mbalimbali mpaka Kuwa kituo cha Bora cha cha kikristo cha Television duniani.

Wawili hawa mtu na mumewe wamefanikiwa kuacha alama duniani kazi imebaki kwako na kwangu, Bwana ametoa na Bwana Ametwaa. 

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.