June 8, 2016

KANISA KATOLIKI KULIOMBEA TAIFA AMANI.


Kanisa Katoliki Tanzania kesho litatumia maadhimisho ya kongamano la Ekaristi Takatifu kuliombea Taifa amani.


Kongamano hilo linaloanza kesho, litahitimishwa Jumamosi, linafanyika kitaifa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza.
Hayo yamesemwa na Askofu Msaidizi wa kanisa hilo Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini.

Askofu Kilaini ametoa wito kwa waumini na watu wote wenye mapenzi mema, kuungana na wakristo wakatoliki wengine duniani, kuliombea Taifa amani na matumaini kwa watu waliokata tamaa.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.