July 2, 2016

NJIA ZA KUISHI NA VIDONDA VYA TUMBO(ULCERS)

NJIA ZA KUISHI NA VIDONDA VYA TUMBO(ULCERS)
 
Kama una vidonda vya tumbo, matibabu yako yatategemea sababu ya vidonda vya tumbo. Kama ni bakteria H.pylori, dawa za kuua na kuondoa bakteria hutumiwa.

Mambo yafuatayo yatakusaidia kuishi vizuri ukiwa na 'Vidonda Vya Tumbo'

1. Acha kutumia kahawa na chai, kwa maana vitu hivi huongeza kiwango cha asidi kinachotengenezwa na tumbo lako.Unaweza tumia chai ya mitishamba 'Herbaltea' kama mbadala.

2. Kunywa maziwa na ule vitokanavyo na maziwa kama maziwa mgando 'Yoghurt',jibini 'Cheese'. Maziwa hufikiriwa kufunika utumbo na kupunguza athari za asidi ya tumboni.

3. Jitahidi kupunguza uzito kama uzito umezidi na hauendani na kimo chako.

4. Kula walau kidogo mara kwa mara. Hii itasaidia kupunguza athari za asidi inayotengenezwa na tumbo.

5. Acha au kunywa vileo siku maalumu tu kwa maana unywaji wa pombe mara kwa mara hutonesha kwenye vidonda vya tumbo vinavyotaka kupona.

6. Epuka matumizi ya viungo vya vyakula kwa maana hufanya hali kuwa mbaya zaidi.

7. Acha kuvuta sigara/tumbaku/bangi. Uvutaji wa sigara utakuweka kwenye hatari zaidi ya kuanza vidonda vipya na kuzuia vidonda vingine visipone.


By Richard Edward

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.