• Isikupite Hii

  July 25, 2016

  Askofu Gwajima amjibu Yusuf Makamba, aliyemuita muongo.

  Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amemjibu Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Yusuf Makamba aliyemtuhumu kuwa ni mwongo, akisema leseni yake ni ya kuendesha magari makubwa siyo vibajaji na maguta.

  Soma: Askofu Gwajima Asema Mazito Kuhusu Serikali Ya Jk Na Kumshauri Mh. Magufuli. (+audio)

  Akihubiri katika kanisa lake jana, Gwajima bila kutaja jina la Makamba, alisema: “Siwezi kushughulika na vigari vidogovidogo nyie mnanifahamu, nina leseni ya kuendesha semi trailer …nadhani mmenielewa,” alisema huku waumini wake wakimshangilia.

  Juzi, Makamba aliwaeleza wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM kuwa, Askofu Gwajima ni kiongozi wa dini lakini ni mwongo na kuwa uongo huo unawaudhi hata waumini wake ambao ni wanachama wa chama hicho.