July 12, 2016

TANZIA: MWIMBAJI MAARUFU AFIWA NA BABA YAKE MZAZI.

Muimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini Kenya, Gloria Muliro amepatwa na pigo maishani baada ya kufiwa na baba yake mzazi. 
Muimbaji huyo ambaye anajiandaa na mzunguko (tour) wa Twende Jerusalem na GoTell kuanzia tarehe 1-7 Agosti kisha kuunganisa mzunguko mwingine, ameandika taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Facebook, akieleza kusikitishwa na taarifa hizo Jumamosi ya tarehe 9 Julai.

Tunawaombea wafiwa wote faraja itokayo kwa Mungu. BWANA ametoa na BWANA ametwaa, jina lake na lihimidiwe.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.