July 27, 2016

BASI LA UDA LAGONGA TRENI KARIAKOO - AJALI.

Basi la UDA lenye namba za usajili T 696 CVP limegonga treni katika eneo la Kamata Jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo  wakati Basi hilo likotokea stendi ya Gerezani Kariakoo kuelekea Mbagala na kuua mtu mmoja na wengine zaidi ya 45 kujeruhiwa.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Ernest Matiku amesema majeruhi wamepelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu.
Hata hivyo, hakuweza kumtaja jina mtu huyo aliyefariki dunia.

"Ni kweli ajali imetokea kuna kifo cha mtu mmoja na watu wengi wameumia sana" amesema Kaimu kamanda huyo.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.