Featured Posts

July 2, 2016

ASKOFU GWAJIMA NI MGONJWA, NDIYO MAANA HAKUTOKEA MAHAKAMANI JANA.

Peter Kibatala wakili wa Askofu Josephati Gwajima ambaye ni Askofu mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima jana aliiomba mahakama kuahirisha tarehe ya kusikiliza kesi inayomkabili askofu huyo sababu anaumwa.

Kibatala aliiambiadai mahakama Kisutu kuwa kutotokea kwa mteja wake jana kulitokana na yeye kuwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Tazama: Picha 4 Za Helicopter Ya Askofu Gwajima Wa Kanisa La Ufufuo Na Uzima.

Wakili huyo aliwasilisha madai hayo jana katika Mahakaama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Syprian Mkeha Hakimu Mfawidhi anayesikiliza kesi hiyo inayomkabili Askofu Gwajima.

Mahakama ilikubali ombi hilo na kwamba kesi hiyo itatajwa tena 2 Agosti mwaka huu.

Katika kesi hiyo Askofu Gwajima anadaiwa kutoa lugha ya matusi dhidi ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu wa Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam.

Askofu Gwajima anadaiwa kufanya tukio hilo kati ya 16 na 25 Machi, mwaka 2015 katika Viwanja vya Tanganyika Packers Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.