July 27, 2016

RAIS HOLLANDE KUKUTANA NA VIONGOZI WA DINI BAADA YA KASISI KUUAWA.

Rais wa Ufaransa atakutana na viongozi wa dini mbalimbali nchini humo, kuonesha mshikamano wa kidini baada ya kasisi mmoja kuuawa.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande atakutana na viongozi madhehebu ya Kikristo, Kiislamu, Kiyahudi na mabuda baada ya watu wenye itikadi kumuua kasisi huyo ndani ya kanisa lake.

Awali Rais wa Ufaransa alisema tishio la magaidi linaloikabili bara Ulaya kwa sasa, halijakuwa kubwa kiasi hicho.

Ameelezea azma yake ya kushinda ugaidi, lakini akaongeza kuwa, polisi tayari wana nguvu ya kutosha kukabiliana nao.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.