July 13, 2016

GOODLUCK GOZBERT, CHRISTINA SHUSHO, ROSE MUHANDO NA ANGEL BENARD KUITIKISA DAR.

Mwanamziki wa Injili Goodluck Gozbert kutoka jijini Mwanza, atakuwa akizindua rasmi DVD yake mpya Iitwayo IPO SIKU jumapili ya Tarehe 17.7.2016. Uzinduzi utafanyika katika kanisa la TAG City Christina Centre (CCC) upanga, Poster jijini Dar es salaam kuanzia saa saba kamili mchana.

Goodluck Gozbert atasindikizwa na waimbaji wakubwa kama mwanadada Angel Benard, Christina Shusho na Rose Muhando. 

Kiingilio Mlangoni ni Shilingi 20,000/= huku Clouds media Group kupitia kipindi chake cha Redio cha Gospel Trax ndio waandaaji wakuu wa tukio hili. 

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.