July 21, 2016

USHUHUDA WA BISHOP MOSES KULOLA KUHUSU JEHANAMU ALIPOCHUKULIWA 1966.

Mungu alimuonyesha tena jehanamu na baadhi ya watu anao wafahamu waliotupwa humo. Alieleza jinsi alivyo huzunika sana. Ingawa ushuuda huu aliutoa ikiwa imepita zaidi ya miaka 50, Mzee kulola alikuwa akitokwa na machozi. Hapa anaeleza katika kitabu chake, Anasema hasira ya moto ule ilimfanya atetemeke, akaanguka na kuzimia.

Alipozinduka akamuona mtu aliyejitokeza akilia kwa huzuni nyingi. Alipomtazama alimtambua kuwa alikuwa ni Mchungaji wake aliyekuwa amefariki kitambo. Yule Mchungaji alimuomba Mchungaji kulola ampelekee maji maana alikuwa akiteseka kwa ule moto. Wakati akishangaa kumuona Mchungaji huyo akiwa motoni maana hakutegemea gafla. Akamuona Mama yake mzazi aliyekuwa amefariki mwaka huo 1966. Naye alikuwa akiomboleza sana na kulia kilio cha kuunguruma akisema.


Soma: Historia Fupi Ya Maisha Ya Marehemu Askofu Moses Kulola.


"Mwanangu usikubali kuja huku, mimi najuta nilidhani Ukristo wangu utanifaa-ole wangu mwanangu. Mwanangu Moses geuza njia ili usije huku. Mimi nakufa milele nikiwa hai kutokana na Mchungaji huyu akujitolea kutupa njia ya uzima. Ewe mwanangu mwanangu Moses nihurumie nihurumie mwanangu. Niletee maji mwanangu nawaka moto huu mkali. Nenda kawaambie wanangu wasije katika Ukristo kama wangu. Kawaeleze upesi"


Moses aliposikia hayo kutoka kwa Mchungaji na kwa Mama yake alizimia kwa huzuni pale pale wakaondolewa.


Ushuuda huu upo katika kitabu kinachoitwa 

Dr.Moses kulola 

Muasisi na askofu mkuu wa kwanza eag(t)
Kimeandikwa na 
Christine john hongoke (phd)
2015.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.