July 18, 2016

MUDA NI SASA.! USIOGOPE KUANZA, WALA USIOGOPE KUKOSEA.

Hakuna aliesema ujasiliamali/uwekezaji ni kitu chepesi. Iwe ndo kwanza umepata wazo lako, iwe ndo kwanza umepata mtaji au umeshaanza biashara yako. Hivyo basi kabla hujakata tamaa tuinue vichwa na tupitie nukuu mbali mbali zenye ualisia katika maisha yetu ya kila siku.

1. "USIONE AIBU PALE UNAPOKOSEA ILA JIFUNZE NA UANZE TENA"  - Richard Benson

Ni wangapi ukata tamaa pale wanapokosea. Jiulize mtu kama REGINARD MENGI hakuwahi kosea pindi anaanza kutimiza ndoto yake ya ujasiliamari?  

Binadamu hukosea ila tunachukua maamuz gani baada ya kukosea ndo kinachotufanya tutofautiane. Mfano wengine hukata tamaa kabisa baada ya kukosea ila wengine hujifunza kupitia makosa.

KUMBUKA: kwa kila kosa ulilofanya jifunze kwamba umegundua kitu ambacho siku nyingine hupaswi kukirudia.

Mfano chukulia Reginard Mengi alifanya makosa 50 pindi anaanza harakati zake za ujasiliamali. Ila kupitia makosa hayo Bw. Mengi aligundua vitu 50 ambavyo havipaswi kufanyika katika swala zima la ujasiliamali/uwekezaji.

Je hii leo ni wangapi wamefaidika na wamefanikiwa kupitia ushauri na mbinu nzuri walizopata au kujifunza kupitia Bw. Mengi ?. 

FUNZO: Haijalishi ni mara ngapi umekosea na hakuna atakaekujua wala kukujali wakati unakosea ivyo cha muhimu ni kujifunza kupitia makosa tunayofanya sisi na makosa wanayofanya wale wanatuzunguka ili kutimiza ndoto zetu. Hapo kila mtu atakuona na kukujua jinsi gani ulivyo na bahati katika maisha.

Mwalimu Alphonce Mustapha. 0659 232 385

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.