July 26, 2016

'FISI' ALIYEFANYA NGONO NA WATOTO MALAWI AKAMATWA.

Raia mmoja wa Malawi alionekana katika habari moja ya BBC akihusishwa na tambiko la usafishaji wa wasichana wadogo kupitia kushiriki ngono nao amekamatwa.

Eric Aniva amekamatwa kufuatia agizo la Rais Peter Mutharika kulingana na mkurugenzi wa mawasiliano ikulu ya Rais, Bright Molande aliyezungumza na BBC, Molande amesema kuwa  kutokana na uovu huo Aniva atashtakiwa kwa kukiuka haki za watoto.

Soma: Unajua Ni Kwanini Masanja Mkandamizaji Ni Tajiri? Siri Iko Hapa (+picha10)

Aidha aliongeza kuwa Rais amechukizwa na yaliofichuliwa katika habari hiyo na ameapa kukabiliana na tamaduni hiyo. Mtu aliyetajwa katika habari hiyo ambaye alifanya mapenzi na zaidi ya wasichana 100 pia imebainika kuwa alikuwa na virusi vya ugonjwa wa UKIMWI.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.