July 9, 2016

Hii ndio adhabu ya kosa la kufanya mapenzi ya jinsia moja.

Kamanda wa Polisi kanda maalum Dar es salaam Simon Sirro aliesema:

"Hili kosa lipo muda mrefu, ukienda kwenye sheria za adhabu kwa nchi yetu kufanya mapenzi kinyume cha maumbile ni kosa la jinai na tumekuwa tukiwakamata watu"

"Kilichokuwa kinakosekana ni suala tu la taarifa lakini ukipatikana hukumu yake ni kubwa inategemea na hakimu, kama sikosei ni kuanzia miaka miaka mitano, sita mpaka saba jela, hili sio kosa la miezi miwili jela"  alisema Kamanda Simon Sirro.