August 6, 2016

JE UNATUNZAJE MIKONO YAKO!!

 JE UNATUNZAJE MIKONO YAKO!!

Mikono tunaitumia sana kuliko kiungo chochote kile, katika kazi zetu za kila siku, kusalimiana na watu, kushika vitu. Mikono iko katika hatari sana ya kupata maambukizi ya magonjwa na vile vile ngozi ya mikono na kucha kuchakaa haraka. Unaweza kuona jinsi ilivyo na umuhimu wa kutunzwa vizuri sio kwamba tu ivutie bali pia kulinda afya yako. Zingatia mambo yafuatayo;

Nawa mikono mara kwa mara

Ukiamka asubuhi kitu cha kwa kabla ya kishika na kufanya chochote nawa mikono kwanzwa, ukitoka chooni, kabla ya kula, ukimaliza kufanya usafi, ukirudi nyumbani kabla ya chochote kila nawa mikono itasaidia sana kuweka mikono yako safi na kuzuia kusambaa kwa vijidudu vinavyoleta magonjwa. Usipende kuchangia taulo ya kukaushia mikono.

Tunza kucha vizuri

Hakikisha kucha haziweki uchafu kwa ndani, pia unaweza kukata kucha katika urefu wa wastani ili iwe rahisi kuzisafisha na wewe mwenyewe usipate shida kujisafisha ukioga. Pia kucha ndefu sana si salama wakati wa kuandaa chakula kwani zinabeba uchafu haraka sana. Pia kama unaosha watoto ukiwa na kucha chafu ni rahisi sana kuwapa magonjwa.

Fungus wa mikononi

Kama mikono yako iko sensitive ukishika maji tu unapata fungus, unatakiwa umuone daktari mara moja wala sio kitu cha kupuuzia, maana una hatarisha afya yako na wengine.

Kuwa na mikono laini na kuondoa ukavu

A- Kila ukinawa hakikisha unapaka lotion au mafuta ( Vaseline, mafuta ya nazi nk) itafanya mikono isipauke na ngozi isikakamae.

B- hata kwa wiki mara moja, kwanza weka maji ya uvuguvugu katika beseni yakuweza kuzamisha mikono,tia chumvi kijko kidogo nusu, limao kijiko kikubwa kimoja, kisha loweka kwa dakika 10 mikono yako kisha isugue taratibu kwa kutumia kitaulo laini kama dakika 5, kisha ikaushe na paka mafuta ya nazi au olive, au glycerine kwa kutumia pamba uku unaisugua taratibu mpaka uone imekua laini. Itasaidia kuondoa weusi katika mikono, sugu na kuifanya iwe laini.

Angalizo

Si vizuri kumshika mtoto mchanga wewe mama mwenyewe na watu wengine kabla ya kunawa mikono, watoto wadogo wako ktk harari ya kuambukizwa harak pa magonjwa.

Kitu cha kwanza watu wanacho notice kwako ni sura na cha pili ni mikono, na sababu hiyo wengi hudhani uzuri wa mikono ni kupaka rangi kucha, au kuvaa pete za kuvutia nk. Wakati kucha zimejaa uchafu kwa ndani, na mtu anaosha mikono akitaka kula tu. Uzuri wa mikono uko katika usafi na matunzo ya mikono yako

By Richard Edward 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.