Featured Posts

August 12, 2016

BARNABA: MIMI NI PASTOR, NIMEBARIKIWA, NINA MPANGO WA KUFUNGUA KANISA LANGU. (+VIDEO)

Miongoni mwa wasanii walioguswa yaani haipiti dakika au saa lazima utaona anapost kuhusu dini kwenye mitandao yake ya kijamii ni msanii Barnaba, ambae alizungumza na Ayo TV juu ya mikakati yake ya kufungua nyumba ya ibada (Kanisa).

Video: Barnaba Boy Akiimba Live Wimbo Wa Ambwene Mwasongwe - Upendo.

"Mimi ni Pastor ambae najitegemea mimi kabla sijawa msanii nilikuwa nasoma sana masuala ya dini lakini sifikiri kuwa Pastor bali nitaifanya kazi ya Mungu mpaka pale mauti yatakaponikuta na ndio maana nimebarikiwa vitu vingi ni msanii naimba nawatungia wasanii nyimbo zao"– Barnaba

"Nafikiri kufungua Kanisa langu na nitawapa watu waliendeshe mimi mwenyewe kwahiyo siku mwenyezi Mungu akibariki ndoto zangu basi lazima nitafanikishe hili sio lazima mkoani popote pale nitaangalia japokuwa asilimia 75 mkoani"– Barnaba

Tazama video hapa chini.
By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.