August 8, 2016

EMMANUEL MBASHA AWEKA WAZI JUU YA MAHUSIANO YAKE NA FLORA MBASHA.

Mwanamuziki mahiri nchini Emmanuel Mbasha siku ya Jana kupitia East Africa Television akiwa sambamba na mtangazaji Sam Misago aliitambulisha rasmi video ya wimbo wake wa Haribu Mipango ya Shetani.

Mbasha alikuwa mgeni wa kwanza kuingia katika kipindi cha Weekend Show akiwa na lengo la kuitambulisha video yake hiyo mpya iliyotengenezwa na Director Pablo na Audio imetengenezwa na mtayarishaji nguli nchini Mtu Mzima Kameta.


Kama ilivyokuwa matarajio ya wengi swali kubwa ambalo Sam Misago alikuwa akilirudia rudia mara kwa mara ni kuhusu uhusiano alionao na mke wake Flora Mbasha.

Soma: Tabia 30 Za Mwanamke Anayeweza Kukufaa Katika Maisha Yako.

Kuhusu hili Emma hakutaka kabisa kuyaongelea maisha ya ndoa yake kupitia television, lakini kutokana na presha ya maswali ya Misago ilibidi Mbasha aweke wazi kuwa kwa sasa hawasiliani na mkewe Flora japokuwa amekiri kuwa kwa upande wake hana mpango wa kuoa kwa sasa bado yuko single.

Mwanamuziki huyo alipoulizwa nini hasa kilipelekea yeye kutotaka na kukimbia interviews na vyombo vya habari kwa muda mrefu Emmanuel Mbasha alisema kwa kipindi kile cha kesi yake mawakili wake hawakutaka afanye hivyo, ila kwa sasa yuko huru mara baada ya kushinda kesi hiyo na akamshukuru Mungu na watanzania kwa kumumbea.Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.