Featured Posts

August 16, 2016

Huyu ndiye mwimbaji ambaye nyimbo zake zinakubalika zaidi na watu wa imani zote.

 HUYU NDIYE MWIMBAJI AMBAYE NYIMBO ZAKE ZINAKUBALIKA ZAIDI NA WATU WA IMANI ZOTE.
Linapokuja suala la mwimbaji ambaye nyimbo zake zinakubalika na watu wa aina zote, dini bila kusahau imani basi Ambwene Mwasongwe ameshika kombe katika kukubalika kutokana na nyimbo zake licha ya kuwa visa vya kweli vinavyowatokea watu lakini pia amekuwa akitoa ama kufundisha jamii namna ya kuishi kwa umoja na upendo ikiwemo kusameheana.

Ambwene ambaye mpaka sasa ana album tatu ambazo kila mmoja zina ubora wake wa ujumbe, ameonyesha kukubalika hata kupitia mitandao ya YouTube ambako kumezoeleka watu kukosoa waimbaji binafsi ama wahusika walio wengi lakini ni tofauti kwa Ambwene ambaye amekuwa akitiwa moyo na kupewa ushauri namna gani anavyoweza kufanya huduma yake kwa ubora zaidi na pia nyimbo zake kuendana na mahudhui ya video anaporekodi.

Ukiacha suala zima la nyimbo na ujumbe, lakini pia sauti ya Ambwene ni ya kipekee kwakuwa anaijulia vyema, si rahisi kumkuta mwimbaji huyu akipayuka ama kuimba katika hali ambayo inawaachia watu mashaka kwamba katika note aliyoimbia basi atamalizia vibaya kama ilivyo kwa waimbaji wengi wanaopenda kupayuka katika uimbaji wao. Mfano wa kupendwa kwa mwimbaji huyu ni pamoja pale mwimbaji Barnabas wa bongofleva alipoamua kuimba wimbo wa Ambwene kwenye moja ya maonyesho yao ya muziki. Lakini pitia pia kwenye mtandao wa YouTube usome namna watazamaji wanavyompongeza mwimbaji huyu.