August 9, 2016

MCHUNGAJI AWATAKA VIJANA WASIOE WASICHANA WAVIVU, WASICHANA WASIOJUA KUPIKA.

Mchungaji Enoch Adejare Adeboye kutoka nchini Nigeria ametoa wito kwa wavulana na makapela wengine wasioe wasichana wasiojua kupika.

Mchungaji Enoch Adejare Adeboye ambae ni msimamizi wa kanisa liitwalo Redeemed Christian Church of God, alitoa wito huo wakati wa hotuba zake kanisani humo, ambazo pia hutangazwa kwenye televisheni.

"usioe msichana ambae hajui kupika!Mchungaji Enoch Adejare Adeboye amewasisitizia mabwana harusi watarajiwa huku akiongeza ' "usioe msichana eti kwa sababu tu anaweza kuimba! Oa msichana anaemuabudu Mwenyezi Mungu, anaeweza kutekeleza maombi kwa Mwenyezi Mungu kisawasawa! Kama hawezi kufanya maombi kwa mda wa saa moja, usimue, usioe msichana mvivu! Usione asiyejua kupika, kwani utakuwa kila siku unakula mahotelini? Huwezi kumudu hizo gharama za kula kwenye migahawa kila mara ?"

Soma: Tabia 30 Za Mwanamke Anayeweza Kukufaa Katika Maisha Yako.

Ujumbe huo ambao umerekodiwa kwenye ukanda wa video sasa uko juu kwenye chati za mitandao ya kijamii baada ya kusambazwa na wengi walioskia.

Baadhi wametoa maoni yao kupitia facebook na twitter, na ni bayana kuwa wanaoufanyia mzaha ujumbe huo, huku wengine wakiona kama uchochezi dhidi ya wanawake au kuingilia maswala ya ndoa za watu lakini pia wapo ambao wanamuunga mkono kwa dhati mhubiri huyo.Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.