August 1, 2016

Hizi ndizo sifa za mume bora 'husband material'.

Kama wewe ni mwanamke na haujaolewa na upo kwenye mauhusiano na mwanaume ambaye haujafunga naye ndoa basi zingatia hili, linaweza kukusaidia na kukupa nuru nzuri ya ndoa bora yenye tija katika maisha yako ya mahusiano.

Chagua mwanaume bora kwa kutizama utashi wake na mawazo yake chanya, mwanaume bora ni yule aliyekuzidi utashi, tabia nzuri pamoja hekima na busara na mwenye mapenzi ya dhati kwako.

Soma: Sifa 7 Za Mwanamke Wa Kuoa (Wife Material).

Mwanaume anayekufaa ni yule anayekujali na kukuheshimu, mwanaume bora ni yule anayekupa mawazo ya kesho akiwa leo, mwanaume anayekufaa ni yule anayekufuta machozi na asiyekuliza kila siku.

Tengeneza mwanaume wako bora, anza naye kwenye maisha ya chini mkipeana faraja na matumaini ya kutengeneza ndoa bora na yenye mafanikio, na mauhisiano yenye afya yaliyo na mapenzi matamu na bora, usipende wanaume wa wanawake wenzio mtengeneze handsome wako.

Mwanaume bora hata kama hana pesa daima huwa na hazina ya mawazo na ndoto zenye matumaini ya kuwa na malengo mazuri baadaye.

Achana na wanaume maarufu wengi wao hawana mapenzi ya dhati wanapenda kuwatumia wanawake kwa tamaa zao za mwili.