Featured Posts

September 12, 2016

BI HILLARY CLINTON AUGUA GHAFLA

 BI HILLARY CLINTON AUGUA GHAFLA

Mgombea Urais kutoka chama cha Democratic Hillary Clinton amekutwa na ugonjwa wa kichomi baada ya kuugua katika tukio la kuwakumbuka wahanga wa shambulio la septemba 11.

Daktari wake Lisa Bardack amesema kuwa bi Clinton amekutwa na ugonjwa huo tokea Ijumaa.

Amesema pia Clinton aliongezeka joto na kuishiwa na maji mwilini katika tukio hilo la kuwakumbuka wahanga wa shambulio la septemba 11.

Clinton aliondoka mapema, picha zilizowekwa mtandaoni zinamuonesha akisaidiwa na msaidizi wake, huku akitaka kuanguka alipokaribia kwenye gari, lakini baadae bi clinton alitokea kwenye nyumba ya mwanae na kuwaambia waandishi wa habari kuwa anajisikia vizuri.

Awali mgombea Urais kupitia chama cha Republican Donald Trump alionesha wasiwasi juu ya afya ya hasimu wake.

Katika shughuli hiyo majina karibu elfu tatu ya wahanga wa shambulizi la Septemba 11 yalisomwa.


By Richard Edward 


Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.