September 21, 2016

Umuhimu wa kuandika husia wa mwisho.

 UMUHIMU WA KUANDIKA HUSIA WA MWISHO.
Inashauriwa kwa kila mtu mwenye familia hasa kwa wale wenye watoto, kuandika husia wa mwisho. Lengo la makala hii sio kukupa taratibu na kanuni za kisheria juu ya uandishi wa husia, bali ni kukupa dondoo muhimu za uandishi wa husia wa mwisho pamoja na faida zake. 

Kama unataka kujua zaidi juu ya taratibu na kanuni za kisheria kuhusu uandishi wa husia, tembelea ofisi yoyote ya wakili wa serikari iliyopo karibu na wewe.

Ni wakati gani sahihi wa kuandaa husia wa mwisho?

Kutokana na utaratibu unaopendekezwa wa kuupitia husia wako angalau mara moja kila mwaka, na hasa baada yamatukio makubwa kama kufunga ndoa, kuzaliwa kwa mtoto au kifo cha mtu aliyetajwa ndani ya husia huo. Hii inamaana kuwa husia unaweza kwandaliwa wakati wowote wa maisha yako na kupitiwa kwa kadri miaka iendavyo, ili kufanya mabadiliko mbalimbali.

Faida za kuandika husia wa mwisho.

Husaidia kujibu maswali yahusuyo matakwa yako kwa kipindi cha kifo chako.

Huakikisha kuwa watoto wanao kutegemea wanapata urithi wao kwa kadri ya matakwa yako.

Pia kupitia husia unapata nafasi ya kumteua mlezi wa watoto wako, hasa kama itatokea ukafariki ghafra na mzazi mwenzako.

Soma: Mambo muhimu ya kufanya asubuhi ili ufanikiwe.

Husia wa mwisho husaidia kuepusha migogoro ya kifamilia, hususani pale taratibu mbalimbali za kimila zinapohusishwa.
Pia husia unasaidia kuhalalisha baadhi ya taratibu ikiwa kama mjane ataolewa na mtu mwingine.

Ni jambo muhimu kutembelea ofisi yoyote ya wakili iliyopo karibu nawe ili kujua kama mambo uliyo yaandika yako ndani ya kanuni na taratibu zinazotakiwa kufuatwa katika uandishi wa husia.

Baadhi ya mambo muhimu yanayotakiwa kuwekwa katika husia wa mwisho;

Orodha ya watoto na majina yao kamaili.

Mtu atakayepewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa husia (Anaweza kuwa mwanasheria).

Mlezi wa watoto hasa kama wazazi watafariki wote kwa pamoja.

Mgawanyo wa mali.

Mgawanyo mwingine kutokana na hali ya mtu binafsi.