September 26, 2016

Kampuni hii ya israel inaweza kudukua simu yoyote ile.

Kampuni moja ya Israel inayowasaidia polisi kudukua simu za washukiwa wa uhalifu nchini Israel Cellebrite, imesema kuwa inaweza kudukua simu yoyote aina ya smartphone. 

Kampuni hiyo iligonga vichwa vya habari mapema mwaka huu wakati ilipodaiwa kuwasaidia maafisa wa ujasusi nchini Marekani FBI kudukua simu aina ya Iphone iliotumiwa na muuaji wa San Bernardino. 

Cellebrite sasa imeieleza BBC kwamba inaweza kuingia katika simu yoyote ya smartphone. Lakini imekataa kusema iwapo inasambaza teknolojia hiyo kwa serikali za kiimla. 

Wiki iliopita kampuni hiyo ilialikwa katika hoteli ambayo maafisa wa polisi kutoka kote nchini Uingereza walionyeshwa vifaa na programu zinazoweza kutoa data ya simu za wahalifu.