• Isikupite Hii

  September 22, 2016

  Mfahamu mwigizaji wa filamu ya Yesu ambaye watu wengi hudhani kwamba ni Yesu.

  Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni nesi ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon, ndoa yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.

  Soma: Historia Fupi Ya Maisha Ya Mchungaji Antony Lusekelo, Mzee Wa Upako.

  Aliigiza filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya kuitazama akiwa na miaka 30, baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza (screen test) kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji.

  Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama yeye (Brian) atafaa kwenye kumwigiza Yesu, lakini anasema alifanikiwa, baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza, sauti yake na mambo mengine, ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa muongozaji.

  Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo na kuweza kumfahamu vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina gani.

  Soma: Historia Fupi Ya Maisha Ya Jennifer Mgendi.

  Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian amesema, walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie kwani amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo lakini anasema alikuwa anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa akizipata na kuendelea kuigiza ingawa wakati huo nasema alikuwa mkristo jina wa kanisa katoliki, alikuwa anauwalakini kuhusu mafundisho na huduma ya Yesu kwa ujumla, siku moja wakati anaigiza alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja alishika mkono wake kumbe alikuwa na mapepo alimuombea na mapepo yalimtoka mwanamama huyo.