October 13, 2016

Kama wewe ni mke wa mtu jiepushe na haya.

 KAMA WEWE NI MKE WA MTU JIEPUSHE NA HAYA
Leo nazungumza na wanawake zaidi ingawa naamini pia mada hii itawasaidia wanaume. Kwa namna moja au nyingine, wanaweza kuwasaidia wake zao, migogoro itapungua ndani ya nyumba.

Isikupite Hii: Mambo 6 Ya Kuzingatia Ili Uishi Vizuri Na Mkwe Wako.

Kwa hakika kila mtu anatambua thamani ya ndoa. Kumkubali mtu awe mume au mke wako, lazima uwe tayari kuwa na maisha mapya. Unatoka katika maamuzi ya binafsi na kwenda kwenye maamuzi ya pamoja.

Kabla ya ndoa, mwanamke anajiamulia mambo yake. Anapoingia kwenye ndoa, mambo mengi wanaamua pamoja na mumewe. Ratiba zinabadilika. Aina ya marafiki wanabadilika, haimaanishi uwatenge kabisa, hapana. Namna ya kuwasiliana nao inabadilika.

Kunakuwa na mipaka fulani kati ya maisha ya ndoa na yale ya kabla. Ule utani uliozidi mipaka unapaswa kupungua. Kama walikuwa wanazoea kufika nyumbani kwako, kuingia hadi chumbani kwako, mkakaa kwenye kitanda kupiga stori, unapoolewa hutakiwi kuruhusu jambo hilo.

Hapo ndipo kwenye msingi wa mada hii. Kuna watu wanaingia kwenye ndoa huku kwa kujua au kutojua wanajikuta wakifanya mambo ya kijinga. Wanashindwa kujitambua. Wanashindwa kuendana na muktadha wa ndoa.

Mke anajikuta akifanya mambo yaleyale ambayo alikuwa akiyafanya kabla ya ndoa. Mfano; utakuta mwanamke alikuwa na utani wa uliopitiliza na marafiki. Marafiki hao wanaweza kuwa wa kike au wa kiume. Yeye anaendelea kuwatania na wao kumtania.

Isikupite Hii: Je Wewe Ni Baby Number 1 Kwa Mwenzi Wako??

Mazoea ya kuitanababy’ au majina mengine ya kimahaba yanayofanana na hilo. Kutaniana vitu vya kijinga katika simu anaendelea nayo pasipokujua kama anapaswa kuviacha.

Anashindwa kuelewa kwa kufanya hivyo anawarahisishia kazi marafiki hao kufanya mambo ya ajabu yatakayoweza kuhatarisha ndoa yake.

Hutakiwi kuruhusu tena mazoea ya kutumiana picha kwenye mitandao, eti mnataniana. Mwanaume asiye mumeo anakuomba picha, umtumie eti halafu akuambie umependeza. Huo ni ujinga. Unaporuhusu kufanya vitendo hivyo jua kabisa unatoa mwanya kwa huyo unayemtumia kukutongoza.

Wewe ni mke wa mtu, una sababu gani ya kuitana baby, mpenzi au majina mengine yanayofanana na hayo na mtu ambaye si mume wako? Una sababu gani ya kumtengenezea mtu mazingira ya kujirahisisha?

Usijichekeshe kwa mwanaume asiye mume wako. Unapozungumza na mwanaume asiye mumeo, usitumie lugha ambayo haina staha. Kufanya hivyo kunamfanya unayezungumza naye akuone hujiheshimu. Kama hujiheshimu unampa ruhusa ya kukutongoza maana anaona unatongozeka.

Kuishi kwa maigizo nao ni ujinga mwingine ambao mwanamke hapaswi kuufanya. Hupaswi kuishi kwa kuiga marafiki zako. Unapokuwa kwenye ndoa wewe na mumeo ndiyo mnaunda ‘serikali’ yenu. Hupaswi kutaka kuvaa kama marafiki zako ambao hawajaolewa wanavyovaa

Isikupite Hii: Unawafurahisha Vipi Wazazi Kipindi Cha Uhai Wako!!

Unapaswa kuvaa mavazi ya heshima maana wewe sasa ni mke wa mtu. Haimaanishi kwamba usipendeze lakini vazi unalovaa liwe na staha. Likutofautishe na madada poa wanaojiuza barabarani. Usifanane sana na wale wadada ambao hawana ndoa.

By Richard Edward 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari makala juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.