• Isikupite Hii

  October 5, 2016

  MUIMBAJI WA GOSPEL AFUNGUKA ALICHOAMBIWA NA RAIS KWENYE MKUTANO WAO WA SIRI.

  Muimbaji wa gospel wa nchini Kenya, Bahati amefunguka kile alichoambiwa na rais Uhuru Kenyatta baada ya kufanya naye mazungumzo kwenye Ikulu ya nchi hiyo wiki hii.

  Bahati alizua gumzo mwezi uliopita wakati alipokuwa akitumbuiza kwenye sherehe za Chama cha Jubilee kwa kitendo chake cha kuwainua kwenye viti viongozi wakubwa wa nchi hiyo akiwemo rais na makamu wake na kukaa yeye pamoja na kufanya mzaha na wake wa viongozi hao kitendo ambacho baadaye muimbaji huyo aliomba radhi.

  Kupitia mtandao wake wa Instagram, muimbaji huyo ameandika maneno aliyoambiwa na rais Kenyatta baada ya kufanya naye mazungumzo, "I Promise to give you 100% Support in Your Journey to Greatness, Count On Me Bahati!!!" Almost Shed a Tear when PRESIDENT UHURU KENYATTA said this to me Minutes Ago at State House Nairobi. WHO’S LIKE MY GOD???.”

  Wasanii wengine wanaonekana kukubalika kwa rais Kenyatta ni Sauti Sol.

  By Chief Hope 

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

  Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.