• Isikupite Hii

  October 18, 2016

  MAMBO HAYA MATANO '5' YATAKUWEKA KARIBU ZAIDI NA NDOA YAKO.

  1. MUOMBEE
  Hili sio tu kwamba litakukumbusha kuhusu mema ya Mungu kwako, bali pia itakufanya uyajua mahitaji ya mumeo ya siku hiyo na kumuombea ili afanikiwe katika mahitaji yake.NDOA

  2. DAIMA MBUSU MNAPOKUTANA NA KUAGANA
  Huu ni ukaribu wa kimwili na kihisia ambao huwakumbusha mume na mke kuhusu ndoa na muungano wao. Lifanye hilo kuwa mazoea yako ya kila siku, unapoondoka mbusu, unaporudi mbusu tena.

  Isikupite Hii: Kama Wewe Ni Mke Wa Mtu Jiepushe Na Haya.

  3. MPIGIE AU MUANDIKIE UJUMBE MFUPI WA SIMU ANGALAU MARA MOJA KWA SIKU
  Mnaweza kupeana taarifa namna siku inavyokwenda. Mnaweza kujadili kuhusu mahitaji yoyote wakati wa jioni na kuhakikisha kuwa kila mmoja wenu amejumuishwa katika mikakati yenu.black couple muslims

  4. ANGALAU DAKIKA 5 ZA MAZUNGUMZO HURU
  Iwe asubuhi au usiku, daima mahusiano yoyote yanahitaji mazungumzo. Zimeni televisheni, zimeni simu zenu na mzungumze. Linaweza kuwa gumu, hasa mkiwa na watoto wadogo, lakini tafuta namna ya kulifanikisha hilo. Kama ukiwa na jambo lako unapata muda wa kulifanya bila kujali upo ‘bize’ kiasi gani, kwa nini usipate muda kwa ajili ya mwenza wako?black couple muslim.

  Isikupite Hii: Mambo Yatakayo Kusaidia Kama Umeachana Na Mwenzi Wako

  5. MKUMBATIE ANGALAU KWA SEKUNDE 30
  Kabla hujaelekea kazini au unaporejea nyumbani au unapoelekea kitandani, mbusu mwenza wako, kwa maana jambo hilo litawapa hisia tamu na maridhawa za kimwili, kiroho na kiakili. Tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa kumbatio hupunguza shinikizo la damu, lakini pia hukuunganisha na mtu unayemkumbatia. Mgusano wa kimwili unapaswa kuwa zaidi ya tendo la ndoa. Kwa kukumbatiana kila siku, nyote mtaweza kujihisi kuwa mnathaminiwa na kupendwa.

  By Chief Hope 

  Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

  Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.