October 11, 2016

Msanii wa gospel wa kenya apondwa kwa kumgeza diamond.

Msanii wa gospel wa Kenya, Will Paul Msafi amejikuta kwenye kitimoto baada ya mashabiki wake kumponda kwa kugeza uvaaji wa Diamond.

Willy ambaye humchukulia Diamond kama role model wake, alipost picha inayomuonesha akiwa kwenye uchukuaji wa kile kinachoonekana ni video yake ijayo, akiwa amevaa koti jekundu lenye drafti na rangi nyekundu, blue na nyeupe.

Pia alikuwa amevaa kofia ya soksi nyeusi, miwani, jeans na viatu vyeusi pamoja na saa na cheni.

Pamoja na kupendeza, tatizo limekuja kuwa kwamba hizo ni aina ya nguo alizokuwa amevaa Diamond wakati alipoenda kwenye interview kwenye kipindi cha Jahazi cha Clouds FM siku chache kabla picha za Willy.

Mashabiki wengi wamemkosoa msanii huyo kwa kuendelea kuwa nakala ya Diamond katika mambo mengi.