October 18, 2016

Tabia 3 za watu wanaokubalika sana na jamii.

1. Tabia ya kujenga tabasamu.
Tafiti nyingi zinaonyesha tabasamu ni kitu muhimu sana katika mahusiano yoyote yale yawe ya kimapenzi au kawaida. Kwa mfano, tabasamu huwa ni kichocheo cha kuwavuta wengi kusikiliza au kutambua umuhimu wa mtu anayetoa tabasamu hilo.


Pia tafiti hizo zinaendelea kuonyesha kila unapotasamu inasaidia kuwasisimua wengine kujaribu kukusikiliza. Hiyo ikiwa na maana kwamba hakuna mtu ambaye anapenda kumsikiliza mtu aliyenuna nuna. Ni lazima uwe na tabasamu fulani ili usikilizwe.
Kampuni nyingi zenye mafanikio kwa kujua hili, ndio maana zimeajiri watu wenye nyuso za bashasha au tabasamu pale mapokezi. Hivyo, Kama unataka kukubalika katika jamii, jifunze namna ya kutengeneza tabasamu zuri litakalo wavuta wengine kwako.
2. Tabia ya kusaidia wengine.
Mara nyingi watu wanao kubalika na jamii kwa sehemu kubwa, ukiwachunguza utagundua ni watu wa kusaidia watu wengine pia. Matatizo au changamto za jamii huyachukulia kama yao. Hivyo kila wakati hushirikiana na jamii zao kuweza kutatua yale yaliyo muhimu.
Kutokana na tabia hiyo ambayo wamejijengea, huwasaidia sana kuweza kuwa watu waliokubalika katika jamii kwa sehemu kubwa. Ni kitu ambacho hata wewe unaweza ukakifanya ili kuweza kuvuta mvuto kwa jamii yako hasa unayoishi.
3. Tabia ya shukrani.
Watu wanaokubalika na jamii na kupendwa na wengi maisha yao yametawaliwa na shukrani. Sio watu wazito sana kushukuru. Kila wanachokipata au pale wanaposaidiwa ni rahisi kwao kuweza kusema ansante mara moja.


Kwa kawaida shukrani yoyote haina gharama. Anza leo kujifunza kushukuru kwa mambo madogo madogo. Wape shukrani ndugu zako waliokutembelea au hata yule aliekupigia simu. Kwa jinsi utakavozidi kufanya hvyo itakusaidia kwako wewe uweze kukubalika kwa jamii yako.