December 25, 2016

AJALI YAUA PADRI NA WAUMINI WATANO.

Watu sita wamefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso eneo la Kanegere, Kata ya Bukandwe, Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.

Ajali hiyo imetokea  jana saa 9.30 alasiri.

Habari zilizopatikana usiku huu, zinadai kuwa miongoni mwa watu waliofariki ni Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Kahama ambaye aliwabeba abiria wanaosemekana ni waumini wa kanisa hilo ambao baadhi yao pia wamefariki dunia.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Salum Ndimu amekiri kupokea maiti wanne na  majeruhi wanane.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.