December 13, 2016

SOMO LA FURSA KUTOKA KWA WATU WALIOFANIKIWA

 SOMO LA FURSA KUTOKA KWA WATU WALIOFANIKIWA
Kwanza anatakiwa kusikiliza #FursaKumi, lakini pili lazima ajitambue yeye, bila Nyota Ndoto kujua yeye ni mwanamuziki mzuri au ana kipaji cha kuimba leo isingefikia hatua ya msanii Nyota Ndogo kutoka, nadhani kikubwa wengi tunakosa kujitambua, kutojua tuna nini nguvu yetu ipo wapi naamini kila mtu ana kipawa na ‘talanta’ aliyozaliwa nayo “Alisema Ruge Mutahaba.
“Wengi hatujui ‘talanta’ tulizozaliwa nazo, kuna mtu anajua kuchora vizuri lakini hajawahi kufikiria kuwa ni ‘designer’ mzuri kwa sababu hakuna mtu aliyemsaidia kumwonyesha anaunganishaje hivi vitu ni kujaribu kujifunza kujitathimini, kujifahamu” Aliongeza Ruge Mutahaba.
“Tunaona madalali, ni madalali wa nyumba wangapi wanatumia ‘Instagram’ kufanya biashara zao, shughuli zao za kazi zote tunazozungumza ziko kwenye ‘contacts’ za simu, kwa kweli wanafanya kazi nzuri sana, ‘smart phone’ inafanya kila kitu kwa sasa hivi” Ruge Mutahaba
Tazama Video Hapa chini...
By Richard Edward

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.