Featured Posts

December 17, 2016

Haya ndiyo mambo ambayo watanzania huyatafuta sana mtandaoni.

Kampuni ya Google imetoa ripoti ya mambo ambayo Watanzania tumetafuta sana mtandaoni mwaka 2016.

Maelezo mengi ambayo tumeyatafuta yameelekea kwenye masuala ya afya, biashara fedha, burudani na mambo ya kijamii. Cha kwanza ambacho watu wengi walitafuta sana mtandaoni ni matokeo ya darasa la saba 2016, ukifwatiwa na mtandao wa burudani Beka Boy.

Vilevile mtandao wa kubet kuhusu matokeo ya mechi za mpira wa miguu unafahamika kama Mkekabet.

Matokeo ya kidato cha nne 2016, pia ni moja ya mambo ambayo yalitafutwa kwa wingi pamoja na Maelezo kumhusu Mtanzania mwanamuziki Hekima Raymond.

Vitu Ambavyo watu walitaka kujua

Ripoti zinasema Watanzania wengi walitaka sana kujua jinsi ya kuweka tone la dawa jichoni, ikifuatwa na jinsi ya kuwapata wawekezaji na wafadhili.

Vilevile walitaka kujua sana jinsi ya kukuza nyusi na pia jinsi ya kujua mwanamke atajifungua tarehe gani.

Kukoroma pia ipo katika listi Watanzania wengi inaonyesha wanataka kujua jinsi ya kuacha kukoroma.

Kujua maana/Tafsiri

Katika maneno ambayo Watanzania walitafuta sana maana, nambari tatu kuna neno la kushangaza ‘Bae’.

Mambo yaliyotafutwa sana Tanzania 2016.
1. Matokeo ya darasa la saba 2016
2. Beka boy
3. Mkekabet
4. Salehe jembe juni 26 2016
5. Malazi Arusha
6. Euro 2016
7. Matokeo ya kidato cha nne 2016
8. Yinga media
9. Muungwana
10. Hekima Raymond.

Walichotaka kujua sana kufanya.
1. Jinsi ya kuweka tone la dawa jichoni
2. Jinsi ya kupata wawekezaji/wafadhili
3. Jinsi ya kukuza nyusi
4. Jinsi ya kujua tarehe ya kujifungua
5. Jinsi ya kuacha kukoroma
6. Jinsi ya kufanya cd kuweza kuifungulia kompyuta
7. Jinsi ya kuomba na ubani
8. Jinsi ya kupika danish na croissant
9. Jinsi ya kuanzisha kiwanda cha chokoleti
10. Jinsi ya kujua iwapo mtoto amegeuka

Ni nini.
1. Furaha kamili/upeo wa furaha ni nini
2. Malengo ni nini
3. Bae maana yake ni nini
4. Elimu rasmi ni nini
5. Ndoa ya wake wengi ni nini
6. Hesabu ya jumla ni nini
7. Matumizi ya pesa ni nini
8. Soko la kubadilishana sarafu za kigeni ni nini
9. Mfumo ni nini
10. Ghala ni nini