December 16, 2016

Hii ndiyo list ya watu 20 wenye nguvu zaidi Duniani - Forbes.

Jarida linalofatilia maisha ya watu maarufu duniani FORBES, wamenifikishia hii list nyingine ya mwaka 2016 ya watu 20 wenye nguvu ya ushawishi zaidi duninia. List hii imebeba majina ya viongozi wakubwa akiwemo Rais wa taifa lenye nguvu duniani, Urusi “Vladimir Putin” aliyeshika nafasi ya kwanza.

Vladimir Putin ameendelea kuongoza list hiyo ya Forbes ya watu wenye ushawishi huku Rais wa Marekani anayemaliza utawala wake mwezi January 2017 Barack Obama, jina lake likionekana kwenye nafasi ya 48 kwenye list hiyo.

Umaarufu wa ghafla wa Rais Mteule wa Marekani Donald Trump, umemtoa kwenye nafasi ya 72 mpaka nafasi ya 2 nafasi ambayo inamuweka mashakani Rais Vladmir Putin wa Urusi kuendelea kuitetea nafasi yake kwa miezi mingine 12.

Rais wa China Xi Jinping yuko kwenye nafasi ya nne, akiwafuatiwa kwa ukaribu na kiongozi mkuu wa makanisa ya Roman Catholic duniani, Papa Francis.

Forbes wamesema kuwa list hii huandaliwa kila mwaka ikiwa na majina ya watu mashuhuri kwenye upande wa Siasa, Biashara na masuala ya dini.