December 29, 2016

Jennifer Mgendi kuvunja ukimya kwa albamu mpya pamoja na filamu.

Msanii mkongwe wa nyimbo za Injili nchini, Jennifer Mgendi baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu anajipanga kuachia albamu yake mpya iitwayo 'Nyuma ya Mlima'.

Muimbaji huyo ambaye amewahi kutamba na wimbo Mchimba Mashimo, Nalia na nyingine nyingi, amesema kuwa ameamua kuachia albamu hiyo kama zawadi ya kuwatia moyo mashabiki wake wanaopita katika magumu mbalimbali.

Isikupite Hii: Je Wajua Jennifer Mgendi Alifunga Ndoa Mwaka Gani? Soma Hapa.

"Nina kila sababu ya kufikisha ujumbe ambao Mungu ameweka moyoni mwangu kwa walimwengu juu ya uweza wa Mungu na kwamba atatuvusha katika magumu yote,"

Aliongeza, "Albumu hii ni mwanzo wa ujio wa filamu yangu mpya ya Baba Jackie ambayo imewasilishwa na wimbo wa Tamaa Mbele,".

Baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albumu hiyo ni pamoja na Tamaa Mbele (Baba Jackie), Penda Unapopendwa, Yesu ni Wathamani, Mitihani ya Maisha na Ninamshukuru Adui.

By Chief Hope

Jiunge Na Tim Heaven Sasa!
 

Kupitia FacebookTwitter na instagram ili kupata habari, makala juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.