Featured Posts

December 15, 2016

Magonjwa 6 yaliongoza kuua watu wengi zaidi Duniani mwaka 2016.

Tukiwa mwishoni mwa mwaka 2016, kuna mambo mengi tumeyashuhudia kama ajari, vifo vya wapendwa wetu, milipoku ya magonjwa mbalimbali, vita na taabu nyingi sana ambavyo vimechukua maisha ya watu wengi sana.

Ukiwa umekaa nyumbani mbele ya Tv yako unaweza ukaona jinsi watu wanavyolalamika sana kuhusu magonjwa kama Kipindupindu, Ebola, Kansa ya Matiti na kadhalika lakini utapigwa na butwaa utakapojua hayo magonjwa yanaua watu wachache sana.
  
Isikupite Hii: Hii Ndio Mikoa Inayoongoza Kwa Maambukizi Ya Virusi Vya Ukimwi.
  
Shirika la afya la umoja wa mataifa 'WHO' linaonyesha riport ya magonjwa nguli ambayo yanaua sana na yanategemea kuua zaidi miaka ijayo kulingana na uhalisi wa maisha ya sasa.

Magonjwa haya kwa nchi za afrika zamani yalikua hayapo kabisa lakini sababu ya sisi watu weusi kuanza kuiga mifumo ya kimaisha ya nchi zilizoendelea yaani kwa kuiga vyakula vyao, madawa yao, na mfumo mzima wa maisha

Magonjwa hayo ni kama ifuatavyo.

1. Magonjwa ya moyo 'Coronary heart disease'.
Ripoti la shirika la afya duniani inaonyesha kwamba watu milion saba na laki nne wanauawa na ugonjwa huu  kila mwaka sawa 13.2% ya vifo vyote duniani. Nchini Marekani tu kila mwaka watu laki sita wanauawa na ugonjwa huu hivyo kuufanya ugonjwa hatari zaidi nchini humo na duniani kwa ujumla.

2. Kiharusi 'stroke'.
Ugonjwa wa Kiharusi umeua watu Milioni Sita na Laki Saba ikiwa ni 11.2% ya vifo vyote duniani kulingana na repoti ya shirika la afya duniani.

3. Magonjwa ya kubana kifua 'Chronic Obstructive Pulmonary diseases'.
Watu Milion 3.1 hufa kila mwaka kutoka na ugonjwa huu na hii ni asilimia 5.6% ya vifo vyote duniani. 

4. Magonjwa ya yanayoshambulia kifua 'Lower Respiratory Tract Infections'.
Duniani kiujumla ugonjwa huu unaua zaidi ya watu milion 3 kila mwaka na hii ni asilimia 5.5% ya vifo vyote duniani.

5. Kansa Ya Koo Na Kifua.
Kansa hizi zinaua watu milioni 1.6 kila mwaka ni sawa na asilimia 2.9% vifo vyote duniani.
  
Isikupite Hii: Wanawake Waongoza Kuwa Na Virusi Vya Ukimwi Nchini.
  
6. Ugonjwa Wa Ukimwi.
Ripoti za shirika la utafiti wa ugonjwa wa Ukimwi linaonyesha kwamba zaidi ya watu milioni 40 wameuawa na ukimwi tangu ulipingia duniani, zaidi ya watu milioni 2 hufa kila mwaka, na watu 5700 huambukizwa kila siku. kwa sasa watu zaidi ya milioni 60 duniani wanaumwa ugonjwa huu na bara la afrika likiwa limeathirika zaidi kwani asilimia 91% ya watoto wenye virusi vya ukimwi wanaishi afrika.

By Chief Hope

Jiunge Na Tim Heaven Sasa!
 

Kupitia FacebookTwitter na instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.