December 21, 2016

Msichana aliyebakwa mara 43,000, ageuka shujaa - karla jacinto (+video)

Mhanga wa biashara ya usafirishaji watu aliyebakwa mara 43,000 hadi kufikia umri wa miaka 16 baada ya kuchukuliwa akiwa na miaka 12, amebadilisha maisha yake kusaidia watu wengine.


Karla Jacinto, kutoka Mexico, anadai kuwa alilazimishwa kufanya mapenzi na walau wanaume 30 kila siku kwa zaidi ya miaka minne akiwa mtoto.Alichukuliwa akiwa na miaka 12 baada ya kurubuniwa na kupelekwa Guadalajara, ambako alilazimishwa kufanya kazi kama changudoa. Aliokolewa mwaka 2008 kwenye operesheni maalumu huko Mexico City.Sasa akiwa na miaka 24 – baada ya miaka mingi aliyoitumia kusahau aliyopitia, amegeuka kuwa mtetezi wa haki za binadamu. Karla sasa anasafiri duniani kusaidia wahanga wengine wa utumwa wa kimapenzi na pia ameshakutana na Papa Francus kuzungumzia suala hilo.