December 19, 2016

Sababu 4 zinazopelekea upendo kupungua\kufa kwa wanandoa.

1. UONGO.
Hakuna kitu kibaya kama uongo kwenye mapenzi, uongo wa aina yoyote ile si mzuri kwa wanaopendana kwa dhati kwa sababu huweza kupunguza mapenzi na uaminifu kwa kiasi kikubwa sana miongoni mwa wanaopendana hasa kama mmojawapo akigundua kuwa mwenzi wake ni muongo/anamdanganya.
  
Isikupite Hii: Hizi Ni Dalili 5 Zinazokuruhusu Kuvunja Uchumba!
  
Kuna vitu vingine hata kudanganyana haileti maana wala haina tija kwa hiyo kuwa mkweli kwa mpenzi wako kwa lolote lile ni jambo jema sana kuliko kuwa unamdanganya kila siku hadi aje kugundua unamdanganya itakuwa matatizo na unaweza kusababisha kuachana.

2. USIRI WA KUPITILIZA.
Miongoni mwa vitu hatari pia kwenye mahusiano ni pamoja na hili la usiri wa kupitiliza. Kama una vitu moyoni na upo kwenye mapenzi/mahusiano bora kabisa si vizuri kuvificha na hasa vile vinavyohusiana na mapenzi yenu moja kwa moja. 

Ni kweli kuna vingine huwezi kumwambia kwa sababu havina mahusiano ya moja kwa moja na mahusiano yenu ila kuna vingine ni lazima avijue ili kutoleta ugomvi au matatizo hao baadae.

3. ANA-CHEAT/ANA MTU MWINGINE.
Hakuna kitu kinauma kwenye mapenzi kama kugundua kuwa Yule unayempenda tena kwa dhati na kumjali kwa kila kitu halafu yeye kumbe ana mtu mwingine zaidi ya wewe.

4. DHARAU.
Hii pia huchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza mapenzi kama sio kuyamaliza kabisa. Unapokuwa kwenye uhusiano jitahidi kumpenda mtu wako kwa hali yoyote na usiwe na dharau kwake au hata kwa marafiki zake au ndugu zake au hata wengineo. Hakuna mtu anayependa mtu mwenye dharau hata awe nani.
  
Isikupite Hii: Viashiria Vitano Vinavyokuonyesha Kwamba Hutakiwi Kuingia Kwenye Mahusiano.
   
Na hii huwa mara nyingi inatokea pale mmojawapo kati ya wanaopendana akimzidi mwenzake uwezo iwe kwa cheo, pesa,uzuri  au hata akili na mara nyingi sana inatokea kwa wasichana pale wanapokuwa wapo juu ya wapenzi wao kiuwezo.