January 26, 2017

Historia fupi ya maisha ya Angel Benard. (+video)

Angel amezaliwa tarehe 29/06/1989, akiwa kama mtoto wa tatu katika familia ya watoto sita. Alfred, Consolatha, yeye, Elizabeth, Anjawe na Lufunyo. Ameanza kuimba akiwa na umri wa miaka 6 katika kanisa la Roman Catholic - Tabata Magengeni, akiwa mshirika wa kwaya kuu.

Amesoma Kisutu Primary School, Zanaki Secondary school, Mbezi Beach High School na kuhitimu University of Dar es Salaam.
     
    
Mara ya kwanza kurekodi ilikuwa 2006 akiwa mwanamuziki wa Bongo flavour katika studio ya Serious Records. Kipindi chote hicho alikuwa akiimba mchanganyiko wa nyimbo za dini na za kawaida, mpaka alipokuja kukata shauri mwaka 2007 september 26 katika kanisa la Mito ya Baraka. 

2008 alirekodi album ya kwanza YOTE YALIKWISHA, 2010 alirekodi nyingine iliyoitwa NITAKUABUDU MILELE. 
Amekuwa sehemu ya vikundi mbalimbali kama vile Messengers band, Whispers Band, Glorious Celebration (GWT) na Pure Mission. 
Itaendelea....