January 12, 2017

Mambo 5 yanayorudisha nyuma biashara yako.

1. Kuendesha biashara kimazoea.
Kuamini zaidi katika njia fulani pekee katika kuendesha biashara na kusahau kuwa mahitaji ya wateja yanaweza kubadilika kutokana uhalisia wa maisha kwa wakati husika.

2. Kukosa ubunifu.
Hivi sasa nchini Tanzania, kila mtu anafikiria kuwa Wakala wa Makampuni makubwa mfano: Simu, Bima na Benki. Simaanishi kuwa ni vibaya, lakini ni vyema kujiongezea ubunifu binafsi.

3. Kudharau wateja wapya.
Huku ni Kujisahau au nasema ni kulala fofofo! Ili kuzinduka usingizini, ulizia makampuni haya makubwa  yaliyowahi kuwepo duniani- “Kodak” na “Sony”, yapo wapo? na yanafanya nini kwa sasa? ukilinganisha na uhitaji wa soko na kukua kwa teknolojia.

4. Kuridhika na aina kadhaa za bidhaa/huduma.
Kuamini kuwa bidhaa/huduma fulani ndiyo iliyolishika soko, hivyo hatubanduki hapo.Ni vyema kukidhi matakwa kwa wateja kwa wingi kulingana na uhitaji wao.

5. Kudharau kujihakiki, hakuna malengo ya muda mrefu.
Tambua kuwa kila baada ya mwaka unaitathmini na kuhakiki biashara yako, kinyume na hapo mambo yanabadilika kwa kasi na unaiweka biashara hatarini.Pia weka malengo ya muda mrefu ya biashara yako yakisaidiwa na malengo ya muda mfupi.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 

Kupitia FacebookTwitterInstagram ili kupata habari, makala juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.