January 19, 2017

Unazifahamu zaida za kula chocolates? Soma hapa

Katika hali ya kawaida watu wengi wamezoea kusikia  na kuambiwa kuwa Chocolate si kitu kizuri na kuna sababu nyingi za kukufanya uamini kuwa chocolate si nzuri.

Watu husema inaharibu meno, wengine hudai kuwa inasababisha kisukari na wengine huenda mbali zaidi wakidhani kuwa inaharibu ngozi kutokana na wingi wa mafuta iliyo nayo.

Watoto wadogo ambao wamezoeleka kuwa wapenzi wakubwa wa chocolate ndio huvunjwa moyo na wazazi/walezi wao katika hili.

Ukweli ni kwamba Chocolate si mbaya kwa afya yako na hii inatokana na matokeo ya utafiti rasmi (research) ambayo yamekuja na faida hizi nne ambazo zitakufanya ule chocolate mara nyingi zaidi uwezavyo.

1.Chocolate ni nzuri kwa Moyo wako.
Utafiti unaonyesha kuwa chocolate inaweza kusaidia kupunguza magonjwa ya moyo na hata shinikizo la damu na shambulio la moyo (Heart Attack).

Chocolate nyeusi zimethibitika kuwa na uwezo wa kusaidia moyo ambao umeanza kuathirika na matatizo ambayo yanaweza kukuletea ugonjwa wa kiungo hicho muhimu kwenye mwili wa binadamu.

2.Inapunguza kisukari.
Ni vigumu kuamini lakini ukweli halisi ni kwamba , chocolate inasaidia kuondoa uwezekana wa mtu kupata kisukari.

Watu ambao wamekuwa na kawaida ya kula chocolate walau kipande kidogo mara moja kwa siku kwa muda wa siku tano wanakuwa na uwezo wa kuwa na kinga dhidi ya kisukari kuliko wale ambao hawali chocolate kabisa.

3.Kupambana dhidi ya Msongo wa mawazo (stress).
Tafiti za kisayansi zimethibitisha kuwa chocolate inasaidia kupunguza msongo wa mawazo au stress.

Watu wenye  msongo wa mawazo hushauriwa kula walau gramu 45 za Chocolate kila siku wa muda wa wiki mbili ili kushusha msongo wa mawazo.

Chocolate hushusha kiwango cha Homoni ya Cortisol mwilini, homoni hii huongeza au kupunguza msongo wa mawazo.

4.Chocolate husaidia kujikinga dhidi ya Jua.
Chocolate husaidia ngozi ya mawadamu kujikinga dhidi ya madhara ya miale ya jua.

Flavonoids ambazo zinatumika kutengeneza chocolate zina chembechembe ya vimelea (microorganisms) vinavyoweza kusaidia ngozi na kuikinga dhidi ya miale ya jua